26.Sep.2011     Nikki Mbishi @ TZhiphop.com

Wakati wimbo wake “Sauti ya Jogoo” ukiendelea kujaribu kuamsha Watanzania, bila shaka watu wengi wanataka kufahamu kitu gani hasa kilimsukuma Nikki Mbishi kuandika wimbo kama ule — mashairi mazito yaliyowasilishwa kwa utulivu na mpangilio wa hali ya juu.

Wakati anahojiwa na TZhiphop.com, Nikki alisema haya: “Nilikuwa nawaza kuongelea uhalisia wa tasnia ya siasa Tanzania inavyojenga matabaka — baina ya watu wa ‘chini’ na wa ‘juu’. Na pia nilitaka kuwakumbusha watu majukumu yao kama jogoo awaamshavyo waliolala alfajiri inapojiri.”

Zaidi ya hayo, Nikki aliongelea mambo mengine kuhusu kazi za kimuziki na ndoto zake baada ya miaka mitano. Mahojiano kamili yanapatikana hapa [bofya].

Pia, waandishi wa TZhiphop wamechambua nyimbo “Hisia” (Nikki, Stereo, Suma & One) na “Sauti ya Jogoo” (Nikki ft. Maulo na Bela Kombo). Makala zinapatikana [bofya]:

There are 3 Comments to "Nikki Mbishi @ TZhiphop.com"

  • D.I.E says:

    from punch lines to jogoo nikki mbishi is a quik thinker, ukimsikiliza kwa umakini uta prove that, coz kwa uzoefu wangu rapers wengi wenye uwezo mkubwa wa ku’freestyle huwa wanaandika mashairi mepesi sana, but ukisikiliza hasa jogoo na play boy uta’prove kuwa he is a heavy weight lyrics writer. so all the most better mbishi, but nataka kujua kama ile singo ”the unpeakable” itkuwa kwenye hii the element mixtape au its a solo album project.
    and raia tunataka kujua where exactly mlab is

  • M-Lab says:

    Taarifa zaidi zinafuata. Kuhusu makazi ya studio, cheki ukurasa wa “contact” (kuna link kulia).

  • jobson says:

    yah hippop ni mithili ya mathematics ambapo ufanya ubongo wako ku fikiri. example on creating punch lines’s mtu ana bidi kutunga mistari migumu ambaya c rahihsi mtu kuelewa kiundani zaidi so ni vizuri sana napo ona wasanii wengi wa hippop kutunga mashairi magumu

Write a Comment

News

Artists

Releases

Videos

About

Partners

Contact

Register